MAJALIWA: TUMEDHAMIRIA KUWEKEZA KATIKA ELIMU YA MTOTO WA KIKE

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa mradi wa shule maalumu ya sekondari ya wasichana Ruangwa na amesema kwamba Serikali imeadhamiria kuwekeza katika elimu ya mtoto wa kike kwa lengo la kumuwezesha kutimiza ndoto zake kielimu. Baada ya kukagua mradi huo, Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na maendeleo yake na amewataka waliokabidhiwa jukumu la kusimamia ujenzi